Chama cha wamiliki wa malori wadogo na wakati Tanzania (TAMSTOA) Siku ya ijumaa walikutana na DP World kujadili sekta ya usafiriahaji nchini. Mpango huu uliwakutanisha viongozi wote wa Tamstoa na Chief Commercial Officer kutoka DpWorld ili kujadiliana mambo mbalimbali na changamoto zinazojitokeza katika sekta ya uchuuzi na usafirishaji mizigo kutoka bandarini.
Mkakati ulielezea zaidi katika kuboresha miundombinu na kutoa nadharia potofu kuhusu wasafirishaji wa mizigo kutoka bandarini.
Akiuliza swali ndugu Shabani Chuki ambaye ni mwenyekiti wa Tamstoa kuhusiana na je ni kweli wasafirishaji wadogo hawatakuwa na nafasi ya kutoa mzigo bandarini? Dp World kupitia bwana Aaron George alijibu kuwa kila mwenye kampuni ya usafirishaji iwe ni ndogo au kubwa basi atakuwa na uwezo wa kutoa mizigo bandarini endapo tubatakuwa amesajiliwa katika mfumo
Pia DP World wamejipanga katika kuleta huduma bora ya utoaji mizigo bandarini na pia katika utoaji hudumu kupitia mfumo wa kiteknolojia